Mtambo Wa Mauti

Title

Mtambo Wa Mauti

Author: Ben R Mtobwa | Uploaded by: MoruoKing | 2nd July, 2017


Description

Anaitwa Mona Lisa. Msichana aliyelandana kabisa na ule mchoro mashuhuri duniani wa Mona Lisa. Msichana mwenye sura ya malaika na umbo la malkia. Mona Lisa anafanikiwa kuutikisa ujabali wa Joram Kiango hata anajikuta akiamua kustarehe naye. Lakini pale anapokurupuka usiku wa manene na kumkuta Mona Lisa akiwa maiti, tundu la risasi likivuja damu kifuani mwake, ndipo Joram Kinago anapojikuta katikati ya mkasa mzito, wa kutisha ambao hajapata kukutana nao maishani. Mkasa ambao vitisho vyake vinaongezeka kila dakika hasa pale Mona Lisa aliyekufa jana anapotokea leo, tena katika kila maficho ya Joram Kiango. Na kila anapotokea maisha ya watu wengi, wenye hatia na wasio hatia, yanaendelea kuteketea. Je, Mona Lisa ni binadamu wa kweli, jini au malaika? Ni miongoni mwa maswali ambayo msomaji atajiuliza anaposoma hadithi hii ya kusisimua, hadithi ambayo punde utakapoanza kuisoma, hutotaka kuiacha kamwe hadi tamati.